Raia wa Catalonia leo hii watachagua
viongozi wao wapya, katika uchaguzi ambao serikali kuu ya Uhispania
inaamini utamaliza msuguano wa kisiasa unaoendelea.
Serikali kuu
ya Madrid iliuvunja utawala uliokuwepo awali, baada ya kuandaa kura ya
maoni iliyodaiwa kutofuata kanuni, iliyotaka uhuru wa eneo hilo.Rais wa Catalonia aliyeondolewa madarakani, Carles Puigdemont, amekuwa akiendeleza kampeni zake za kujitenga na Madrid akiwa uhamishoni nchini Ubelgiji kwa kupitia mitandao ya kijamii.
0 comments: