Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema
kuwa mwelekeo wa benki ya Walimu hauridhishi na inawezekana ikafutwa na
kufilisika kabisa.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kuongeza kuwa kati
ya benki 58 zilizopo nchini, benki ya wlimu ni miongoni mwa ambazo zina
muelekeo wa kufutwa.
“Nilialikwa
kwenda kufungua benki ya walimu sijaenda kufungua. Nilitamani kwenda
kuifungua lakini nilipopewa ripoti na BoT nilisikitika. Tuna benki sasa
hivi katika nchi hii benki 58, lakini benki ambazo zina mwelekeo wa
kufutwa na kufilisika na ninyi mmeweka mtaji wenu mojawapo ni benki ya
walimu,” amesema Rais Magufuli.
Rais aliwataka walimu kuhoji namna ambavyo fedha walizoziwekeza zinavyotumika katika kuendeleza benki hiyo na maslahi ya walimu.
“Sitaki
kuwaficha walimu wenzangu. Ni lazima muulize hiyo mitaji mliyoiweka
pale imeenda wapi. Mliowaweka pale wana maslahi ya walimu?,” amehoji
Rais Magufuli.
Aidha
rais magufuli amewahakikishia walimu wote wanaodai madeni yao kwa
serikali kuwa watalipwa mara baada ya uhakiki kukamilika endapo tu
madeni yote ni halali.
“Nataka
kuwaahidi kwamba haya madeni ya walimu, hata kama yangekuwa bilioni
ngapi, Kama ni madeni halali nawahakikishia kuwa nitayalipa yote. Nataka
niwaahidi walimu wenzangu, mara baada ya kazi hii ya uhakiki
kumalizika, wale wote wanaodai madeni halali watalipwa,” alisema Rais
Magufuli.
0 comments: