Thursday, 14 December 2017

WAZIRI MKUU AONGOZA KUAGA MIILI YA ASKARI 14 WA JWTZ WALIOUAWA WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI NCHINI DRC CHINI YA UMOJA WA MATAIFA(UN)

Waziri mkuu, Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo baada ya kuwasili viwanja vya makao makuu ya jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) Upanga jijini Dar es salaam, Desemba, 14 2017 kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa katika operesheni ya kulinda amani nchini DRC, (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kwenye kitabu cha Maombolezo baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao akuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017 kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa kwenye operesheni ya kulinda amani nchini DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam, Desemba 14, 2017 kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 waliouawa kwenye Operesheni ya Ulinzi wa amani nchini DRC.
Askari wa Jeshi la Wananchi la Tanzania(JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa kwenye Operesheni ya Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa(UN) nchini DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

0 comments: