Thursday 14 December 2017

MICHEZO: PSG wataja sababu za Neymar kutotokea uwanjani.

Club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa imeweka wazi sababu za kutokuwa na mpango wa kumtumia mchezaji wao wa kimataifa wa Brazil Neymar wakati wa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Ufaransa dhidi ya Strasbourg.
Kocha wa PSG Unai Emery amethibitisha kuwa hawatokuwa na Neymar wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa wakiwa ugenini dhidi ya Strasbourg kutokana na staa huyo kupewa ruhusa maalum ya kwenda kwao Brazil kushughukia matatizo yake ya kifamilia na atarudi baada ya siku tatu hadi nne.
Hata hivyo Neymar ambaye ni mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa kutokana na kusajiliwa na PSG kwa dau la pound milioni 199 akitokea FC Barcelona, aliukosa mchezo wa weekend iliyomalizika wa PSG dhidi ya Lille uliyomalizika kwa PSG kupata ushindi wa magoli 3-1 kutokana na kutumikia adhabu.

0 comments: