Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema mustakabali wa chama tawala African National Congress upo katika tishio.
Alikuwa anazungumza katika mkutano wa kumchagua mtu atakayemrithi kama kiongozi wa chama hicho.
Rais Zuma amezungumza kuhusu haja ya kuwa na umoja ndani ya ANC, kinachotishiwa na kumeguka.
Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura.
Zuma amesema tuhuma kuwa serikali yake ilishinikizwa na maslahi ya wafanya biashara zitachunguzwa.
Wagombea wakuu wanaopigiwa upatu kumrithi kama kiongozi wa chama hicho ni naibu rais, Cyril Ramaphosa, na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Nkosazana Dlamini-Zuma, mkewe Zuma wa zamani.
Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa.
Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.
Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baad ya kuwepo madrakani kwa miaka 23.
Kikao hicho kinakutanaisha wajumbe takriban elfu tano mjini Johannesburg (BBC SWAHILI)
0 comments: