Saturday 16 December 2017

Wajumbe wa chama cha ANC wakutana kumchagua kiongozi mpya

Chama tawala cha ANC nchini Afrika kusini kinafanya mkutano mkuu kumteua kiongozi mpya wa chama hicho.
Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa.
Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.
Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baad ya kuwepo madrakani kwa miaka 23.
Kikao hicho kinakutanaisha wajumbe takriban elfu tano mjini Johannesburg.
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini anatarajiwa kuhutubia wajumbe wanaohudhuria mkutano huo mkuu.
Wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.
Kivumbi hasa kipo katika Kinyanganyiro cha kumrithi rais Zuma, kama kiongozi wa chama- ni kati ya mkewe wa zamani Bi Nkosazana Dlamini-Zuma -- ambae pia aliwahi kuwa waziri na vilevile alikuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika.
Lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanaomuunga mkono makamu wa sasa Cyril Ramaphosa,
Mvutano huu pamoja na kashfa chungu nzima hasa za rushwa zinazomuandama rais Jacob Zuma zimeongoza hofu za kugawanyika kwa ANC.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili. (BBC SWAHILI)

0 comments: