Dar es Salaam. Uongozi wa Jumuia ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
umesema umekamilisha kuhakiki matokeo ya kura zilizopigwa katika
uchaguzi uliofanyika Desemba 13,2017.
Taarifa iliyotolewa jana Jumamosi Desemba 16,2017 na Idara ya Itikadi na
Uenezi ya CCM imesema uhakiki umefanyika baada ya kupokea malalamiko
kutoka kwa wajumbe wa jumuia hiyo walioshiriki uchaguzi.
Mwenyekiti wa Wazazi, Dk Edmund Mndolwa leo Desemba 16,2017 amesema
matokeo yaliyotangazwa na kumpa ushindi Nuru Bainaga kwa nafasi ya
Wazazi kwenda Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) yanatenguliwa.
Dk Mndolwa amemtangaza Zainab Sige kuwa mjumbe halali wa Wazazi kwenda UWT badala ya Nuru.
“Huu ni mwendelezo wa kuhakikisha kuwa haki inatendekea katika chaguzi za chama na jumuia zake,” imesema taarifa hiyo.
Dk Mndolwa Desemba 13, 2017 alitengua ushindi wa Ngingite Mohamed
aliyechaguliwa kuwa mjumbe wa NEC kutokana na kasoro wakati wa uchaguzi.
Mwenyekiti huyo wa Wazazi, alimtangaza Kitwala Komanya kuwa mjumbe wa NEC kupitia Wazazi (Bara) kuchukua nafasi ya Mohamed.
Mwananchi.
0 comments: