JE ZANZIBAR HEROES KUTWAA CHALLENGE CUP LEO?
Leo Jumapili December 17, 2017 wadau wengi wa soka wanasubiri kuona Zanzibar Heroes watafanya nini nchini Kenya kwenye mchezo wa fainali ya CECAFA Senior Challenge Cup mwaka 2017 ambapo watacheza dhidi ya wenyeji Kenya.
Rekodi zinaonesha kwamba, Zanzibar wameshinda ubingwa wa Challenge mara moja tu, ilikuwa mwaka 1995 walipowafunga wenyeji wa michuano hiyo mwaka huo timu ya taifa ya Uganda kwa bao 1-0. Miaka 22 baadaye, Zanzibar wamefika hatua ya fainali jambo zuri na la kuvutia wanacheza dhidi ya mwenyeji wa mashindano (Kenya) Je watarudia walichofanya mwaka 1995 dhidi ya timu mwenyeji?
Historia inaendelea kutukumbusha kwamba, Zanzibar inatafuta ubingwa wake wa pili kwenye mashindano hayo wakati Kenya wakitaka kuweka rekodi ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya saba. Mra ya kwanza Zanzibar kushinda taji hilo ilikuwa ni 1995 wakati Kenya wameshatwaa kombe hilo mara sita (nafasi ya pili nyuma ya Uganda ambao wameshinda ubingwa huo mara 14)
Makundi CECAFA 2017
Group A: Kenya (wenyeji), Rwanda (Guest), Libya, Tanzania bara, Zanzibar (mechi zilichezwa Machakos) Group B: Uganda, Burundi, Ethiopia, Sudan Kusini (mechi zilichezwa Kakamega)
Kumbuka timu ambazo zimefuzu kucheza fainali (Kenya vs Zanzibar) zote zimetoka Group A, ambapo Kenya waliongoza kundi wakifuatiwa na Zanzibar waliomaliza katika nafasi ya pili.
Road to final
Kenya
Kenya 2-0 Rwanda
Kenya 0-0 Libya
Kenya 0-0 Zanzibar
Kenya 1-0 Tanzani
Zanzibar
Zanzibar 3-2 Rwanda
Tanzania 1-2 Zanzibar
Kenya 0-0 Zanzibar
Libya 1-0 Zanzibar
Nusu Fainali
Kenya 1-0 Burundi
Uganda 1-2 Zanzibar
Failani
Kenya ?? Zanzibar
Kocha wa Zanzibar Heroes Hemes Suleiman ‘Morocco’ amesema, timu yake ipo tayari kwa mchezo wa fainali huku akiamini watapata matokeo bora.
“Karibu wachezaji wote wako vizuri isipokuwa mchezaji mmoja tu (Kassim) na tuliweza kucheza mechi ya nusu fainali bila yeye, tuko vizuri na tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali dhidi ya Kenya.”
“Watu waendelee kutupa support kama ambavyo walifanya kwenye mechi nyingine na sisi tutajitahidi kuhakikisha tunapata matokeo bora. (MUUNGWANA BLOG)
0 comments: