Umoja
wa Mataifa umemwambia Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Joseph Kabila kutimiza ahadi aliyoiweka ya kuachia madaraka na kupisha
uongozi mwingine kuiongoza nchi hiyo hususani wakati huu ambapo nchi
hiyo imejaa migomo na maandamano ya kushinikiza ajiuzulu.
Rais
Kabila mwenye miaka 46, ameiongoza DRC kwa miaka 17 na msimu wake wa
mwisho wa uongozi uliisha tangu December 31, 2016 na akatakiwa aachie
ngazi lakini uchaguzi wa kupata Rais na viongoi wapya umekuwa
ukiahirishwa mara kwa mara.
Suala
hili limesababisha vurugu na maandamano ya raia wa DRC ambao hata hivyo
inaelezwa kuwa wamekuwa wakipigwa na askari polisi jamabo ambalo kwenye
taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa December 31, 2017 imelaani
vikali vitendo hivyo hususani Jijini Kinshasa ambapo watu watano
waliuawa na polisi siku hiyo vya Jumapili kwenye maandamano.
0 comments: