Wednesday 3 January 2018

Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim

Rais wa Marekani Donald Trump amejigamba kuwa kibonyezo chake cha silaha za nyuklia ni kikubwa na kilicho na nguvu zaidi kuliko kile cha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un.
Ujumbe wa Twitter wa Trump ndio wa hivi punde wakati ya majibizano kati ya viongozi wa mataiafa hayo mawili yaliyo na silaha za nyukiia.

Korea Kaskazini inadai kuwa ina silaha za nyulia na inaweza kuishambulia Marekani huku wadadisi wakisema kuwa ikiwa Korea Kaskazini ina silaha za nyulia haibainiki ikiwa ina teknolojia ya kuzitumia.
Kando na kuitishia Marekani, ujumbe wa mwaka mpya wa Kim pia uliwashangaza wengi wakati alisema kuwa alikuwa aayari kwa mazungumzo na Korea Kusini na ange[penda kuituma timu kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini mwezi ujao.
apema wiki hii Kim alionya kuwa kibonyezo chake cha nyuklia kawaida kiko kwenye meza yake.

CHANZO: BBC SWAHILI.

0 comments: