Marekani imetoa kauli juu ya kile
kinachoendelea nchini Iran, kwamba inampango wa kuitisha kikao cha
dharula ina mpango wa kuutaka Umoja wa Mataifa utangaze hali ya hatari
ya kipindi cha mpito katika kikao kijacho cha baraza la usalama la umoja
wa mataifa , wakati ambapo waandamanaji wanaoipinga serikali
wameendeleza maandamano kwa siku ya sita sasa.
Balozi wa Marekani
katika umoja wa mataifa, Nikki Haley, amesema kwamba hali ilivyo nchini
Iran huenda suala hilo likajitokeza katika kikao cha baraza la haki za
binaadamu la umoja wa maifa mjini Geneva.Alitupilia mbali madai ya udanganyifu yaliyotolewa na serikali ya nchi hiyo kuwa maandamano yanayojiri nchini mwake yaliandaliwa na vikosi vya nchi za nje.
Marekani tayari imekwisha chukua hatua ya ya kuitaka nchi ya Teheran kuweka sheria kali zitakazo dhibiti vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii wakati wote wa kipindi hiki cha mpito.
Nayo serikali ya Iaran imetoa tamko la kuwepo kwa mikutano shirikishi ya hadhara leo Jumatano katika maeneo ambayo maandamano yameshika kasi na nguvu zaidi.
BBC SWAHILI
0 comments: