Wednesday 3 January 2018

Simba na Yanga Vitani kesho Mapinduzi Cup

Timu vigogo za Ligi Kuu Tanzania Bara zitatupa karata zake kwa mara nyingine tena kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Yanga itaanza kushuka dimbani saa 10 jioni ikijaribu bahati yake  dhidi ya mabingwa watetezi JKU ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kuzoa pointi tatu.

Timu hiyo ya Jangwani tayari imejikusanyia pointi tatu kwenye mchezo wake wa kwanza baada ya kuichapa Mlandege mabao 2-1.

Simba watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanarudisha matumaini kwa mashabiki wao kutokana na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mwenge. Wekundu wa Msimbazi watakutana na Jamhuri saa mbili usiku.

Hata hivyo Kocha wa Simba, Masoud Djuma alisema kwamba kupata sare mchezo huo ni kutokana na uchovu waliokuwa nao wachezaji kwa sababu wikiendi walikuwa na mechi dhidi a Ndanda FC waliyoubuka na ushindi wa mabao 2-0.

0 comments: