Wednesday 3 January 2018

Saudia Arabia yashutumiwa na wanaharakati

Wataalamu sita wa kujitegemea wanaofanya kazi na baraza la haki za binaadamu la umoja wa mataifa, wameitaka nchi ya Saudi Arabia kuwaachilia wanaharakati kadhaa wa haki za binaadamu walioko kizuizini ama kufungwa tangu mwezi Septemba mwaka wa jana.

Katika taarifa ya pamoja, waliyoitoa wataalamu hao inatanabahisha kuwa zaidi ya viongozi wakuu wa dini wapatao sitini, waandishi vitabu, waandishi habari, wasomi nguli na wanaharakati wamegeuka kuwa wafungwa tangu kipindi hicho.

Katika taarifa hiyo ya pamoja, hawakumjumuisha mhubiri wa mageuzi Salman al-Awdah,mwandishi wa makala na vitabu Abdullah al-Maliki, na Issa bin Hamid al-Hamid wa Shirika la Haki za Kiraia na haki za kisiasa nchini Saudi Arabia.

Kufuatia tamko hilo, hakuna ama hakukuwa na majibu ama tamko la haraka kutoka kwa serikali ya Saudi Arabia, ambayo daima imekuwa ikikana taarifa kuwa kuna wafungwa wa aina tofauti tofauti ikiwemo wale wa kisiasa nchini mwake.

0 comments: