Sunday 25 February 2018

Wajue kiundani wababe wakiarabu watakaokutana na SIMBA SC. Si wa mchezo mchezo
Kaskazini mashariki mwa Misri unapatikana mji wa Port Said. Mji wa Port Said una ukubwa wa kilometa 30 tu sawa na mile 19. Una idadi ya wa watu wasiopungua laki sita. Mji huu ulianzishwa mwaka 1859 wakati wa ujenzi wa mfereji wa Suez. Miaka 61 baada ya kuanzishwa Port Said mwaka 1920 klabu ya Al Masry ilianzishwa.  Klabu ya Al Masry inatumia uwanja wa Al Masry club stadium unaobeba mashabiki 17,000. Uwanja huu inasadikia ulisababisha kusimamishwa kwa ligi kuu Misri mwaka 2012 baada ya vurugu kutokea.
Klabu ya Al Masry inakutana uso kwa uso na klabu ya Simba katika kombe shirikisho. Klabu ya Simba imeweka makazi yake mashariki mwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam. Simba ilianzishwa miaka 16 baada ya Al Masry kuanzishwa mnamo mwaka 1936.  Jiji la Dar Es salaam pia lipo kwenye ukanda wa pwani kama ililivyo kwa jiji la Port  Said ambapo klabu ya Al Masry inapatikana. Jiji la Dar es salaam hapo awali lilijulikana kama Mzizima yaani mji wa afya njema kutokana na hali nzuri ya vyakula hasa hasa shughuli ya uvuvi wa samaki.

Sultan Majid bin said aliamua kutengeneza mji wake ndani ya Mzizima akauita nyumba ya aman yaani Dar (Nyumba) Es saalam (Amani). Kumbe Dar es salam maana yake nyumba ya amani ambapo kinyume chake ni Dar al hard yaan nyumba ya vita. Hapa majiji mawili yanakutana Jiji La Porto lenye vitimbi vya migogoro hasa katika mfereji wa Suez, pamoja na Vurugu za uwanja wa Port Said na jiji la Dar Es Salaam linalosifika kwa utulivu na aman.
Klabu ya Al Masry inaongozwa na kocha mkuu Hossan Hassan ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji nguli wa zamani wa taifa la Misri. Hossan Hassan alizaliwa mwaka 1966 katika jiji la Cairo katika eneo la Helwan ambalo rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser alitangaza eneo hilo kuwa mji wa viwanda. Hossan Hassan ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu taifa ya Misri akiwa na magoli 69 kwenye michezo 169. Anatajwa kama mchezaji bora katika historia ya soka barani Afrika. Anakumbukwa sana kule nchini Uswisi kwa kuitandika klabu ya Celtic magoli manne kwenye mchezo mmoja akiwa na klabu ya Neuchatel Xamax kwenye michuano ya kombe la UEFA.
Pia aliwahi kuichezea klabu hiyo Al Masry kunako mwaka 2004 mpaka 2006. Mnamo mwaka 2008 alipewa kandarasi ya kuionoa klabu hiyo. Alitundika daruga akiwa na miaka 42.
 Awali ya yote ni watoe hofu mashabiki wa Simba ambao wanadhani Al Masry ni klabu kubwa kama akina Al Ahly au Zamalek. Klabu hii haijawahi kutwaa ubingwa ligi kuu Misri tokea ligi hiyo ianzishwe mwaka 1948. ila imejitahidi kumaliza  nafasi tatu za juu kwenye msimamao wa ligi mara sita tu. Licha ya kuwa haina mafanikio makubwa sana ligi kuu lakini ni klabu yenye mashabiki wengi sana nyuma ya al Ahly, Zamalek na Ismalia. Ilikuwa na mafanikio makubwa sana miaka ya 1921 mpaka 1989. Imetwaa kombe la sultan mara 3, kombe la Misri mara moja mwaka 1998, na kombe la shirikisho la Misri mara moja nayo ni mwaka 1992.
Pia imetwaa kombe la kanda ya mfereji wa Suez mara 17 kombe ambalo kwa sasa halipo tena na lilikuwa likijumuisha timu za majiji matatu tu. Kikubwa Heshima kubwa walio nayo ni kuwa imekosa kushiriki ligi kuu miaka miwili tu, walishuka daraja mwaka 1957 mpka 1959 baada ya mgogoro mkubwa kwenye mfereji wa Suez ambapo mapato ya klabu yalishuka na baadhi ya wachezaji kuondoka. Kiwango chao msimu huu sio cha kutisha sana kama cha kama moto walio nao vijana wa Manara. Kwanza wapo nafasi ya 4 kwenye msimamo wao wa ligi wakiwa na alama 42 baada ya michezo 23. Katika michezo kumi ya mwisho ya ligi wameshinda michezo mitano wametoka suluhu michezo mitatu na wamepoteza miwili.
 Nitoe tahadhari, hawa jamaa nao wana balaa lao, wanagawa vipigo kwa timu kubwa na vya magoli mengi. Mnamo tarehe 5 mwezi wa pili walitoa dozi ya magoli manne ugenini kwa klabu ya El Maqasa, wakaliza El Tanta magol sita kwa mbili,  wakaizibua El Nasri ugenini kwa magoli matatu kwa mawili. Pia wakaitandika Zamalek ugenini goli moja.
Katika klabu hii wachezaji wa kuogopwa ni A Bance mwenye mabao matano akiwa na umri miaka 33, pamoja na mshambuliaji Ahmed Gomaa mwenye magoli 11 akiwa na umri wa miaka 29,  Ahmed Sokri kiungo machachari na mkongwe mwenye magoli matano akiwa na umri wa miaka 30, mwingine ni pamoja na Islam Abou Slemma mwenye magoli matano. Ni hayo tu.
 Michezo Hii ndio ratiba ya michuano ya kombe la Europa, Arsenal uso kwa uso na AC Milan
Droo ya hatua ya raundi ya 16 bora ya kombe la Europa League 2017/18 imepangwa Ijumaa hii.

Macho ya mashabiki wengi wa soka yatakuwa katika mechi ya Arsenal ambao wampangwa kuanza ugenini na AC Milan ya Italia. Mechi nyingine ita wakutanisha Marseille dhidi ya Athletic, wakati Atletico Madrid wataanzia nyumbani dhidi ya Lokomotiv Moskva.
Nao Dortmund wamepangwa kucheza dhidi ya Salzburg. Tazama ratiba kamili hapa chini.
Yanga SC yatinga robo fainali Kombe la Shirikisho
Klabu ya Yanga imetinga  robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Majimaji FC, mchezo uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
 Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi kwa pande zote mbili huku Majimaji wakiongoza kumiliki mpira, Nyavu za Majimaji ndio zilianza kuchezewa na Yanga kupitia kwa Pius Buswita katika dakika ya 40.
Katika kipindi cha pilidakika ya 52, Emmanuel Martin alifunga Yanga goli la pili kwa njia ya kichwa, akiunganisha krosi nzuri ya Hassan Kessy, na kufanya matokeo yawe mabao mawili kwa Yanga na sufuri kwa Majimaji.
Goli la kufutia machozi la Majimaji lilifungwa kunako dakika ya 61 ya mchezo na Jaffar Mohammed na kufanya ubao wa matokeo kubadilika kuwa 2-1 hadi mchezo huo unamalizika.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo inakuwa ni timu ya tano kufuzu.
China kuongeza muhula wa Rais Xi Jinping madarakani baada ya mwaka 2023
Chama kinachotawala nchini China kimependekeza kuondoa sehemu katika katiba ambayo inaweka muhula wa rais kuwa mihula miwili ya miaka mitano kila muhula.

Hatua hiyo itaruhusu rais wa sasa Xi Jinping kubaki kiongozi baada ya muhula wake kukamilika, Kumekuwa na uvumi kuwa Bw Xi ataongeza muhula wake hadi kupita mwaka 2023.

Kamati kuu wa chama mwaka uliopita iliboresha nguvu za Xi na kumfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi tangu uongozi wa Rais Mao Zedong.

Fikra zake pia zilijumuishwa katika katiba ya chama, na kwenda kinyume na ratiba hakuna mrithi aliyetangazwa.

Kamati kuu ya chama cha kikomunisti ilipendekeza kuondoa sehemu inayosema kuwa Rais na Makamu wa Rais wa China wanastahili kuhudumu kipindi kisichozidi mihula miwili kulingana na katiba.

Kamati hiyo haikutoa taarifa za kina lakini taarifa kamili zinatarajiwa kutolewa, Hatua hiyo inajiri wakati maafisa ya vyeo vya juu ambao wako katika kamati kuu wanatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu mjini Beijing.

Bw Xi amekuwa madarakani tangu mwaka 2013 na chini ya mfumo wa sasa alistahili kuondoka madarakani mwaka 2023.
Mkuu wa majeshi ya Korea Kaskazini azuru Korea Kusini
Ujumbe wa Korea Kaskazini unaoongozwa na jenerali wa jeshi mwenye utata umevuka na kuingia Korea Kusini kwa sherehe za kufungwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi huko Pyeongchang.

Jenerali Kim Yong-chol analaumiwa kwa kuzamisha meli ya vita ya Korea Kusini mwaka 2010 ambapo wanajeshi 46 waliuawa. Korea Kaskazini inakana kuhusika.

Familia za waathiriwa na wabunge kadhaa wa Korea Kusini walifanya maandamano wakijaribu kuzuia ziara hiyo kwenye mpaka.

Ziara hiyo inafanyika wakati kuna kuboreka kwa uhusiano kati ya Korea hizo mbili, Wakati wa mashindano ya olimpiki Korea Kaskazini na Kusini walitembea pamoja chini ya bendera moja wakati wa sherehe za ufunguzi na baadaye wakawa na kikosi cha pamoja na wanawake wa timu ya magongo.

Hata hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini.

Ujumbe wa Marekani kwenye mashindano hayo unaojumuisha binti wa rais Donald Trump Ivanka, umekana kukutana na maafisa wa Korea Kaskazini.

Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea Kaskazini, Rasi ya Korea imegawanyika tangu vita vya miaka 1950 na pande zote mbili hazijawai kuwa na makubaliano ya mkataba wowote.
Mlinzi wa Simba aanza rasmi mazoezi
Mlinzi wa kati wa timu ya Simba Salim Mbonde amepona majeraha yake na ameanza rasmi mazoezi chini ya Kocha wa Viungo 'Fitness Coach' Mohammed Hbibi kwaajili ya kujiandaa kuanza kucheza.

Taarifa ya klabu hiyo leo imebainisha kuwa mlinzi huyo ataendelea na mazoezi hayo chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo Yassin Gembe na anatarajiwa kuwa kamili kucheza hivi karibuni.

Salim Mbonde alisajiliwa na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili msimu huu ambapo amekuwa akicheza kwa kupishana na walinzi wengine ndani ya timu hiyo wakiwemo Juuko Murshid, Mlipili na Nyoni.

Klabu ya SImba inaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa raundi ya 19 ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC. Mchezo huo utapigwa kesho kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo Simba itaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa kimataifa kombe la shirikisho barani Afrika utakaopigwa Machi 6 mwaka huu dhidi ya Al Masry ya Misri.
Van Gaal kuchukua mikoba ya Antonio Conte?
Kocha wa zamani wa Manchester United, Mholanzi, Luois van Gaal, anatajwa kuwa anaweza akachukua mikoba ya Antonio Conte anayeinoa Chelsea kwa sasa.

Conte amekuwa hapewi nafasi kubwa ya kuendelea kukinoa kikosi hicho licha ya kutwaa ubingwa wa Ligi msimu uliopita.

Kwa mujibu wa jarida la Mirror, linaeleza kuwa Van Gaal anapewa nafasi hiyo, na kama mazungumzo yatakuwa sawa anaweza akatua darajani kufundisha Chelsea.

Conte amekuwa akilalamikiwa na mashabiki wa Chelsea tangu achukue ubingwa wa ligi, huku wengi wakimtuhumu kwanini alimuacha Diego Costa.
Rais Magufulii Azungumzia Tena Kaya 1900 Zilizovamia Uwanja wa Ndege Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amerejea nchini  tarehe 24 Februari, 2018 akitokea nchini Uganda ambako amehudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika jana Mjini Kampala.

Katika uwanja wa ndege wa Mwanza Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella aliyeongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Antony Dialo.

Akiwa uwanjani hapo Mhe. Rais Magufuli amezungumza na wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ambao wamemuomba asaidie kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili uwanja huo zikiwemo mahitaji ya jengo la abiria kutokana na jengo lililopo kuwa dogo, mahitaji ya ujenzi wa uzio wa kuzunguka uwanja na ndege zinazobeba minofu ya samaki kutotumia uwanja wa Mwanza na badala yake kutumia viwanja vya nchi jirani kutokana na ongezeko la tozo ya kodi kwa ndege hizo.

Katika majibu yake Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itafanyia kazi mahitaji ya kujengwa kwa jengo la abiria pamoja na ujenzi wa uzio ili uwanja wa Mwanza uwe na hadhi ya kimataifa na hivyo kuiwezesha nchi kupata mapato zaidi.

Kuhusu changamoto ya ndege za kubeba minofu ya samaki kutotumia uwanja wa Mwanza Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itafanyia kazi jambo hilo na kulitafutia ufumbuzi haraka ili ndege hizo zitumie uwanja huo na kuiingizia nchi mapato.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema anasubiri ripoti ya Wizara ya Ardhi kuhusu wananchi waliovamia uwanja wa ndege wa Mwanza lakini amebainisha kuwa Serikali haiwezi kukimbilia kuondoa kaya zaidi ya 1,900 zinazodaiwa kuvamia eneo hilo na badala yake itaangalia njia bora ya kufanya.

Hata hivyo ametaka wananchi waliopo katika eneo hilo wasiendeleze makazi yao wakati uamuzi wa Serikali unasubiriwa.

“Bahati nzuri Naibu Waziri wa Ardhi upo hapa, kafanyieni kazi changamoto hii na mnipe ripoti” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Baada ya kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza Mhe. Rais Magufuli ameelekea nyumbani kwake Chato Mkoani Geita kwa mapumziko.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
24 Februari, 2018
Kakobe akana kukwepa kodi,asema taarifa za TRA ni za Kisiasa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Followship (FGBF), Zachary Kakobe amekanusha taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kanisa lake linakwepa kodi.

Akizungumza leo Jumapili Februari 25, 2015 katika kanisa hilo lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam Kakobe amewataka waumini wa kanisa hilo kuzikataa taarifa hizo na kwamba zimejaa siasa,ni za kishilawadu

Kakobe ametoa ufafanuzi huo zikiwa zimepita siku nne tangu TRA kutoa taarifa ya uchunguzi katika kanisa hilo na kubaini mambo saba.
Hukumu ya Sugu Kusomwa Kesho February 26
Hatima ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayeshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli itajulikana kesho.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ambayo kesho Februari 26,2018 itatoa hukumu.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari 9,2018.

Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.

Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.

Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.

Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.
Wahamiaji Haramu 83 Wakamatwa Iringa
Zikiwa zimepita siku tatu tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam iwahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela wahamiaji haramu 77 kutoka Ethiopia, wengine 83 wamedakwa mkoani Iringa huku dereva aliyekuwa akiwasafirisha akifanikiwa kutoroka.

Wahamiaji hao walikamatwa wilayani Kilolo mkoani hapa wakiwa safarini kupelekwa Malawi kisha Afrika Kusini.

Hata hivyo katika harakati za kukamatwa kwao, dereva wa lori mali ya mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya alitoroka.

Raia hao wa Ethiopia walikamatiwa katika Kijiji cha Mbigili ambapo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Hope Kawawa alisema walikamatwa juzi saa kumi na moja jioni karibu na bomba la mafuta la Tazama.

Alisema wahamiaji hao walipelekwa kituo cha polisi cha Lugalo na kwamba, kukamatwa kwao kunatokana na taarifa iliyofikishwa Uhamiaji na wananchi.

Alisema maofisa wa Uhamiaji kwa kushirikiana na polisi walipowakamata baadhi yao waliwakuta hali zao ni mbaya kutokana na kukosa chakula kwa siku tatu na pia kuathiriwa na joto kutokana na bodi la lori walilokuwa wakisafiria kuwa la bati. 
“Wahamiaji hawa walikuwa wanasafiri kwenye lori mali ya mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya, dereva alikimbia na hajapatikana lakini uchunguzi unaendelea,” alisema.

Aliongeza kuwa wahamiaji hao watafikishwa mahakamani kesho kujibu mashtaka yanayowakabili.

“Naomba niwaambie madalali wanaosafirisha hawa wahamiaji kuwa mkoa wa Iringa si mahala salama kuwapitisha kwa kuwa tuko makini saa 24 na tukiwabaini hatua kali zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapohisi baadhi ya watu si raia wa Tanzania na wanapowaona watu wasiowatambua. Mtanzania aliyekamatwa akihusishwa na usafirishaji wa wahamiaji hao, Hassan Mwalusanjo alisema hana anachofahamu.

Alisema aliomba lifti katika gari hilo kutoka Tukuyu kwenda Dar es Salaam kununua vifaa vya gari wakati gari hilo lilipokuwa likisafirisha ndizi. Mwalusajo alisema baada ya kushusha ndizi eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, dereva aliondoka na aliporeja alipanda kurejea Tukuyu.

Alisema walipofika Ilula alishuka kula ndipo dereva alipoondoka na gari na aliporejea alimuomba amsaidie kusafisha gari.

“Sielewi chochote nilishangaa kuwekwa chini ya ulinzi baada ya dereva kuniambia nimsaidie kusafisha gari ambako nilikuta makopo ya maji na mifuko ya mikate,” alisema akiwa chini ya ulinzi.’’
 

Ahadi ya FIFA kwa Tanzania baada ya Rais Gianni Infantino kufika Nchini
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeahidi kuendeleza viwanja tisa nchini kufuatia kuongezeka kwa dau la pesa za Maendeleo na Kujiendesha zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kuanzia mwaka 2019 .

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyojadili na Rais wa FIFA Gianni Infantino alipokuwa nchini kwa mkutano wake hivi karibuni.

‘’Rais wa FIFA alieleza kuongeza mara nne ya kiwango cha pesa za maendeleo na kujiendesha walizokuwa wanatoa kwa mashirikisho kama TFF mpaka kufikia Dola Milioni Moja na Laki Mbili na Nusu kwa mwaka na kusema pesa hizo ndiyo zitumike kuendeleza viwanja vya michezo kwani uwepo wa viwanja ndio unaosaidia kukuza vipaji vya soka,’’alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa Rais huyo wa FIFA ametoa msisitizo wa kutokuwa na huruma kwa kiongozi yoyote wa shirikisho atakayekuwa na matumizi mabaya ya pesa pamoja na kufanya udanganyifu kwani yeye yuko mstari wa mbele kupinga ufisadi katika sekta ya maendeleo ya Soka duniani.

Pamoja na hayo nae Rais wa TFF  Bw. Wallace Karia alitoa ufafanuzi wa hali ya kifedha kwa shirikisho na kueleza kufuatia kuwepo na matatizo katika shirikisho hilo .FIFA ilikuwa imesitisha kuwapatia fedha hizo za maendeleo za kujiendesha tangu mwaka 2015 lakini baada ya kuingia uongozi mpya FIFA wameridhika nao na wameshaupa utaratibu wa kufuatilia fedha hizo.

‘’Rais wa FIFA alitueleza kuwa fedha hizo ziko salama nchini Zurich ni kwamba tu hazikuwa zimeruhusiwa kuingia nchini na kwa sasa tumeshaanza mchakato wa kufuatilia fedha hizo kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA hivyo basi tutakapo pata fedha hizo Shirikisho  litaendeleza baadhi ya miradi ambayo tumekwisha iandaa,’’alisema Bw. Karia.

Pamoja na hayo rais huyo alitoa wito wa wakazi wa jiji la Tanga waliovamia eneo linalotarajia kujengwa Technical Center  ya mchezo wa soka  waondoke mara moja kabla hawajachukuliwa hatua.
Mlanguzi wa mihadarati, Washington Prado Álava wa Ecuador, ahamishiwa Marekani
Mwanamume mmoja ambaye anatuhumiwa kuingiza hadi Marekani zaidi ya tani 250 ya dawa za kulevya aina ya cocaine katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, amehamishiwa Marekani kutoka Colombia.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa, Washington Prado Álava, raia wa Ecuador, alikuwa mlanguzi mkuu wa mihadarati kote Amerika.
Pia anasemekana kuamuru kuuwawa kwa majaji, waendesha mashtaka na maafisa wa polisi nchini Ecuador.

Bwana Prado Álava alifahamika nchini Colombia kama Pablo Escobar, wa Ecuador, jina la kinara mmoja sugu wa genge maarufu liitwalo Medellín, ambaye aliuwawa mwaka 1993.
Nchini Colombia, alijaribu sana kujiunga na kundi la mrengo wa kushoto la waasi la Farc, kabla kundi hilo kutia saini na mapatano na serikali ya nchi hiyo, ili kukomesha mapigano.
Waendesha mashtaka nchini Colombia, wanasema kwamba nia yake kuu ilikuwa kupata cheo cha juu ndani ya kundi hilo na kisha kuchukua udhibiti wa sheria ya taifa hilo.
Kundi hilo la Farc lilisababisha uhasama wa muda mrefu sana nchini Colombia kwa zaidi ya miongo mitano.
"Washington Prado Álava anadhaniwa kuwa kiongozi mkuu zaidi wa ulanguzi wa mihadarati katika miaka ya hivi karibuni, na amekuwa akilengwa na Marekani," waendesha mashtaka walisema hayo katika taarifa waliyoitoa.
Bwana Prado Álava, anasemekana kuendesha biashara hiyo yake haramu nchini Ecuador na kisiwani Colombia, pwani ya bahari ya Pacific.
inasdemekana kuwa maboti yake kadhaa inayoenda kwa kasi, yalitumika mara kwa mara kusafirisha Coccaine hadi katikati mwa Amerika na Mexico, na kutoka hapo, dawa hizo za kulevya ziliwasilisha hadi katika mpaka wa Marekani.
Bwana Prado Álava alikamatwa Aprili 2017alipokuwa akisafiri kutembelea familia yake katika mji wa Cali nchini Colombia.
Shirika la Marekani la kupambana na mihadarati USDEA, iliipa utawala wa Colombia na vidokezo muhimu vya ki- intelijensia, iliyosababisha kukamatwa kwake kwa pamoja na wanachama wengine watatu wa genge hilo.
Siku ya Jumamosi, aliondolewa ndani ya gereza alimokuwa amezuiliwa katika mji mkuu Bogotá, na akawekwa ndani ya ndege ili kukabiliwa na sheria nchini Marekani.
Askari 50 walihusika katika operesheni ya kumhamishia Marekani, Utawala nchini Colombia umesema.

Friday 23 February 2018

Kabwe: Tutaendelea kupambana dhidi ya sheria kandamizi Tanzania
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto Kabwe ameachiliwa huru kwa dhamana asubuhi hii baada ya kukamatwa na polisi usiku wa kuamkia Februari 23mkoani Morogoro, karibu kilomita 200 kutoka Dar es salaam.
Sababu ikitajwa ni kufanya mikutano bila kibali alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea viongozi wa chama chao cha ACT Wazalendo maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Alipokamatwa Bw Zitto aliweka ujumbe katika akaunti yake ya Twitter, "Ninasindikizwa hadi kituo cha polisi cha Mgeta wilayani, Mvomero.... Sijaambiwa kwa nini nimekamatwa."
Mbunge Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya shilingi milioni 50 fedha za kitanzania na kudhaminiwa na wakaili wake ndugu Emmanuel Lazarus Mvula.
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alikuwa kwenye ziara ya chama chake mkoani humo.

Ametakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi12, 2018.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Zitto Kabwe na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wamesema wataendelea na ziara ya kutembelea kata zinazoongozwa na chama hicho.
Vile vile Zitto akaelezea katika ukurasa wake wa Facebook " Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo."
 Katika eneo hilo hilo, taarifa za usiku wa kuamkia leo, zinasema mjumbe mwingine kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA ameuwawa. Taarifa zinasema Diwani huyo wa kata ya Namwawala Godfrey Luena alikutwa nyumbani akiwa mauti baada ya kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.
 Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, Jeshi la polisi mkoani Morogoro limethibitisha tukio hilo na Kamanda wa mkoa humo Ulrich Matei amesema chanzo cha mauaji hayo huenda ikawa ni ulipizwaji wa kisasi kutokana na tukio la mauaji ya aina kama hiyo lililowahi kujitokeza miaka ya nyuma.

BBC SWAHILI
Machimbo ya madini ya Tanzanite yazungushwa ukuta Tanzania
Ukuta mrefu unaozunguuka machimbo ya madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani nchini Tanzania, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Tayari wakuu wa vyombo vya usalama, wametembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za kiTanzania isiyozidi bilioni 6.
Na kusisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.
Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, wanasema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.Ugumu wengine walioupata ni uchimbaji katika maeneo yenye miamba.
Kwa upande wao, wakizungumzia usalama baada ya kukagua eneo hilo, wamezungumzia uadilifu katika kulinda eneo hilo.
Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo amesema ukuta uko imara na kwamba hatua ya pili itafuata katika kuuboresha zaidi.

Ukuta wote mpaka sasa umegharimu shilingi bilioni 6 za Kitanzania, umejengwa na wanajeshi

Amesisitiza kuwa ulinzi unahitaji uzalendo zaidi kutokana na Watanzania wakati mwingine kuwa ndio wanaohujumu mali za nchi.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Siro amesema jambo kubwa ni wananchi kuwa na uelewa kwa nini ukuta huo umejengwa.
Baada ya kukamilika kwa awamu hiyo ya ujenzi, awamu ya pili itafuata kuboresha baadhi ya maeneo na kuweka vifaa zaidi vya kiusalama.
Rais wa Tanzania John Magufuli anatarajiwa kuuzindua rasmi ukuta huo, utakapokamilika kwa asilimia mia moja.

BBC SWAHILI


Hiki ndicho Walichoongea Rais Magufuli na Kenyatta Baada ya Kukutana Leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kutatua tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika biashara kati ya nchi hizi mbili.

Marais hao wametoa maagizo hayo leo asubuhi tarehe 23 Februari, 2018 walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Munyonyo mjini Kampala muda mfupi kabla ya kuanza kwa vikao vya mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Kenyatta wamesema wanataka kuona biashara kati ya Tanzania na Kenya inazidi kukua na bidhaa zinauzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote na hivyo kuagiza tofauti zilizojitokeza katika baadhi ya bidhaa zimalizwe.

“Kuna mambo madogomadogo yanakuwa yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka kwa haya yote Mawaziri wa Kenya na Mawaziri wa Tanzania mkae myatatue, sisi hatuna tatizo, mambo mengine madogomadogo mno, mambo ya viatu, nguo, ngano, gesi ni madogo sana, mnatakiwa myatatue nyinyi yasifike kwetu, sisi huku tuko sawasawa” amesema Mhe. Rais Magufuli na kuungwa mkono na Mhe. Rais Kenyatta.

Wametoa maagizo hayo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kaskazini wa Kenya Mhe. Peter Munya.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit katika hoteli ya Munyonyo Mjini Kampala.

Baada ya Mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki inaguswa na hali ya Sudani kusini na ametoa wito kwa pande zinazopingana kumaliza tofauti zao ili wananchi wa Sudani Kusini wajikite kujenga nchi yao.

“Nimemhakikishia Mhe. Rais Salva Kiir kuwa Tanzania ipo pamoja na Sudani Kusini na tunapenda tofauti zinazosababisha matatizo nchini mwake ziishe, sisi Tanzania tupo tayari kufanya biashara na Sudani Kusini, hata chakula kama wanahitaji tutawauzia” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mhe. Rais Salva Kiir Mayardit amesema Tanzania na Sudani Kusini zina uhusiano wa kihistoria tangu enzi ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na kwamba japo kuna vita nchini mwake Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa uhusiano na ushirikiano huo utaendelezwa na kukuzwa zaidi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Gaston Sindimwo.

Mhe. Gaston Sindimwo amemfikishia ujumbe wa Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza kuwa hali ya Burundi ni shwari na Mhe. Rais Magufuli amesema anafurahi kuona sasa wakimbizi wa Burundi waliokuwa wamepata hifadhi Tanzania wameanza kurudi nchi kwao.

Mhe. Rais Magufuli pia amefanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni mratibu wa mazungumzo ya amani ya mgogoro wa Burundi aliyealikwa kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hapa Kampala.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kampala
23 Februari, 2018
Mnyama Simba SC Anoa Makucha yake dhidi ya Mbao
Kocha wa msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema kwamba, sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao
“Tunashukuru tumerudi salama, mechi yetu ilikuwa nzuri hatukutumia nguvu nyingi kwa sababu tulishinda 4-0 hapa ukizingatia tuna mechi za ligi kwa hiyo hatukutaka kujichosha sana, tulichohitaji ugenini ni kutoruhusu goli na sisi tupate angalau goli moja jambo ambalo tulifanikiwa.”
“Kwanza hatuangalii hata huo mchezo wetu na hiyo timu ya Misri, hapa mbele tuna mechi za ligi ambazo ni muhimu kuliko hata hiyo mechi na Al Masri.
“Tunaiandaa timu kwa ajili ya mechi dhidi ya mbao, hiyo Al Masri ukifikika wakati wake tutajiandaa.”
“Mechi dhidi ya mbao ni ngumu lakini ni lazima tushinde kwa sababu hakuna kingine tunachoweza kufanya kwa sababu tukitoka sare tunazidi kupoteza nafasi na sisi hatutaki kupoteza nasfai kwa sababu ndio nafasi pekee iliyobaki kwa Simba kushinda ubingwa.”
Fujo za mashabiki zaua Askari
Askari Polisi mmoja nchini Hispania amefariki kwa mshituko wa Moyo baada kuanguka wakati akijaribu kutuliza ghasia za mashabiki kwenye mchezo wa EUROPA kati ya Athletic Bilbao na Spartak Moscow jana usiku.

Askari huyo wa kiume aliyetambulika kwa jina la Inocencio Arias Garcia, alikuwa na umri wa miaka 50. Baada ya Garcia kuanguka wakati wa vurugu hizo nje ya uwanja wa San Mames,  kabla ya mchezo  alikimbizwa Hospitali lakini tayari alikuwa ameshapoteza maisha.

Shirikisho la soka nchini Hispania RSFF pamoja na Rais wa La Liga Javier Tebas, wametoa pole kwa familia ya Garcia pamoja na kukemea vitendo vya vurugu michezoni huku wakitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia mashabiki waliohusika katika tukio hilo.

Katika vurugu hizo zilizohusisha makundi ya mashabiki wa timu za FC Spartak Moscow na Athletic Bilbao imeripotiwa kuwa mashabiki watatu wa Kirusi na afisa mmoja wa polisi walipelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa.

Katika mchezo huo wa marudiano ulimalizika kwa Bilbao iliyokuwa nyumbani kwenye uwanja wa San Mames kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Spartak lakini imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya kushinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Kauli ya Zitto Kabwe baada ya kuachiwa
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuwataka watu wasirudishwe nyuma kwa vitisho na usumbufu wa sheria kandamizi zinazopelekea baadhi ya viongozi kukamatwa na kuwekwa ndani.

Zitto Kabwe ameweka wazi hayo mara baada ya kuachiwa leo Februari 23, 2018 na kusema kuwa yeye anaendelea na harakati zake ya kuwafikia viongozi na Kata ambazo wananchi waliwachagua viongozi wa ACT Wazalendo.

"Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe ameonyesha kuguswa na muaji mengine ambayo yametokea jana ambapo diwani wa CHADEMA ameauwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali katika mwili wake

"Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia" alisema Zitto Kabwe


Hii ndiyo Orodha kamili ya washindi wa tuzo za BRIT Awards 2018
Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za BRIT Awards 2018 lilihitimishwa Jumatano ya wiki hii, huku mastaa kama Kendrick Lamar, Harry Styles na wengineo wakiondoka na tuzo hizo.

Hii ndiyo orodha kamaili ya washindi wa tuzo hizo kwa mwaka 2018.

British Album of the Year:
Dua Lipa – Dua Lipa
Ed Sheeran – Divide
J Hus – Common Sense
Rag ‘n’ Bone Man – Humour
Stormzy – Gang Signs & Prayer — WINNER

British Male Solo Artist:
Ed Sheeran
Liam Gallagher
Loyle Carner
Rag’n’Bone Man
Stormzy — WINNER

British Female Solo Artist:
Paloma Faith
Kate Tempest
Jessie Ware
Laura Marling
Dua Lipa — WINNER
British Group:
Wolf Alice
Gorillaz — WINNER
London Grammar
The XX
Royal Blood

British Breakthrough:
Dave
Dua Lipa — WINNER
J Hus
Loyle Carner
Sampha

Critics’ Choice Award:
Jorja Smith — WINNER
Mabel
Stefflon Don

British Single of the Year:
Liam Payne – “Strip That Down” featuring Quavo
Jax Jones feat. Raye – “You Don’t Know Me”
Clean Bandit – “Symphony” featuring Zara Larsson
Rag’n’Bone Man – “Human” — WINNER
J HUS – “Did You See”
Calvin Harris – “Feels” featuring Pharrell Williams, Katy Perry and Big Sean
Dua Lipa – “New Rules”
Ed Sheeran – “Shape of You”
Jonas Blue – “Mama” featuring William Singe
Little Mix – “Touch”

International Female Solo Artist:
Taylor Swift
Lorde — WINNER
Bjork
P!nk
Alicia Keys

International Male Solo Artist:
Kendrick Lamar — WINNER
Childish Gambino
Drake
Beck
DJ Khaled
International Group:
Foo Fighters — WINNER
Arcade Fire
LCD Soundsystem
Haim
The Killers

British Artist Video of the Year:
Ed Sheeran – “Shape Of You”
Harry Styles – “Sign Of The Times” — WINNER
Liam Payne Ft Quavo – “Strip That Down”
Little Mix – “Touch”
ZAYN and Taylor Swift – “I Don’t Wanna Live Forever”

Sunday 18 February 2018

Mazishi ya Akwilina kugharamiwa na Serikali

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kugharamia mazishi ya mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji (NIT), Akwilina Akwelina aliyeuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa Februari 16, 2018 wakati wa maandamano ya wafuasi wa CHADEMA wakishinikiza Mkurugenzi wa Uchaguzi Kinondoni kutoa viapo kwa mawakala wa chama hicho.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Februari 18, 2018 na Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Prof Joyce Ndalichako alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

“Serikali imepata pigo kwani inawekeza fedha nyingi kusomesha wanafunzi na marehemu Akwilina alikuwa ni miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, tutagharamia shughuli zote za mazishi ya marehemu hadi atakapopumzishwa katika makao yake ya milele,“amesema Prof. Ndalichako huku akitoa onyo kwa Watanzania kuhusu maandamano.

“Nawasihi watanzania kujiepusha na maandamano na vitendo vyote ambavyo vinaweza kusababisha uvujifu wa amani,“Prof. Ndalichako.

Watu wote 66 waangamia kwenye ajali ya ndege Iran
Watu 66 wameuawa kwenye ajali ya ndege ya abiria nchini Iraan, maafisa wa kampuni wamesema.
Ndege hiyo ya shirika la Aseman, ilikuwa safarini kutoka mjini Tehran kwenda mji wa kusini magharibi wa Yasuf wakati ilianguka kwenye milima ya Zagros kati kati mwa Iran.
Shirika la msalaba mwekundu lilituma kikisi cha uokoaji kweda eneo hilo karibu na mji wa Semirom mkoa wa Isfahan.
Ndege hiyo namba 3704 iliondoka Tehran mwendo wa saa (01:30 GMT) na kutoweka kutoka kwa rada baadaye.

Maafisa wanasema kuwa hali mbaya ya hewa imetatiza jitihada za uokoaji.
Ndege hiyo inaaminiwa kuwa ya miaka 20 iliyotengenezewa nchini Ufaransa.
Ripoti zinasema kuwa wale waliokuwa ndani ya ndege ni abiria 60, walinzi wawili, wahudumu
wawili, rubani na msaidizi wake.
Rais Magufuli aagiza hatua dhidi ya waliosababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwiline
Rais wa Tanzania John Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na kuwachukulia hatua waliosababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji Tanzania, NIT, Akwilina Akwiline.


"Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili," Rais Magufuli aliandika kwenye mtandao wa Twitter.
Mwanafunzi huyo ambaye jina lake na picha vilisambazwa katika mitando ya kijamii alipigwa risasi akiwa ndani ya basi dogo maarufu kama daladala jijini Dar es salaam, siku ya Ijumaa majira ya jioni, ikiwa siku moja kabla ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge la kinondoni kufanyika.

Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na risasi katika harakati za kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha Chadema waliokuwa wakiandamana hadi afisi za tume ya uchaguzi.
Wakati huo huo mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), wamemtaka waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana na tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Akwilina Akwilini.
Taaria zaidi pia zinasema kuwa polisi 6 wamekamatwa kwa tuhuma za kutumia risasi za moto wakati wa uchaguzi mdogo mjini Dar es Salaam.

BBC SWAHILI

Saturday 17 February 2018

Yondani, Ngoma yaongeza nguvu
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.
WAKATI Donald Ngoma na Kelvin Yondani wakirejea katika kikosi cha Yanga, timu hiyo kesho inaondoka kwenda Shelisheli tayari kwa kurudiana na St Louis ikitarajia kuacha wachezaji kumi katika safari hiyo.

Ngoma alianza mazoezi jana asubuhi huku Yondani akithibitishiwa na daktari wa timu hiyo, Edward Bavu kuwa yupo tayari kucheza mechi hiyo ya marudiano itakayochezwa Jumanne ijayo mjini Viktoria, Shelisheli.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, msafara wa Yanga utakuwa na wachezaji 20 kati ya 30 ambao imewasajili kwenye msimu huu.

Wachezaji watatu Buruhani Akilimali, Anthony Matheo na kiungo kinda, Maka Edward wao hawatakuwepo katika msafara kwani majina yao hayapo kwenye usajili wa Caf.

Mtoa taarifa wetu alisema, Thabani Kamusoko naye yupo kwenye hatihati ya kuwepo kwenye orodha ya watakaoondoka kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100 kucheza mchezo huo.

“Wachezaji watakaobaki ni Amissi Tambwe, Ninja (Abdallah Shaibu), Yohana Nkomola na Ngoma, wengine ni Maka, Matheo na (Burhan) Akilimali ambao majina yao hayakupelekwa Caf.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh yeye alisema: “Tumebakisha siku moja kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo ni kesho (leo) halafu tutakuwa na kikosi kamili.

“Ila Ngoma, Tambwe na Ninja hawaendi.” 
Salumu Mwalim afunguka Mawakala wa Chama Chake Kuzuiwa Kuingia
Mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni kupitia Chadema, Salum Mwalimu amelalamikia uchaguzi huo kuwa mawakala wa chama hicho wamezuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kwa wakati.

Akizungumza leo Februari 17, 2018 amesema mawakala wa chama hicho kikuu cha upinzani wamechelewa katika baadhi ya vituo kwa saa mbili hadi tatu.

Mwalimu alitolea mfano Kata ya Hananasifu kuwa mawakala hao wameingia saa 2 asubuhi wakati vituo vyote 613 vya kupigia kura vimefunguliwa saa 1 asubuhi.

Mwalimu ambaye alitembelea kituo cha Hananasifu B, amesema mawakala hawa wamezuiwa baada ya kuelezwa kwamba hawana fomu za halmashauri na wengine zile za kiapo.

"Cha ajabu nimeingia kituo kimojawapo halafu wakala wa chama cha UMD anazo barua zote tangu saa 12 asubuhi wakati huohuo wakala wa Chadema hana barua na nilipohoji wananiambia mbona wakala wa CCM pia hana barua na hajaingia,” amesema Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar,

"Sasa mtu anapoanza kukuuliza mbona na wa CCM hana unaanza kujiuliza maswali mengi kwanini? Mle ndani walivyokaa wamejipanga kufanya wanachokifanya na wao wanajua wanafanya kazi kwa maelekezo ya nani.”

Amedai tatizo kama hilo pia limewahi kujitokeza kata ya  Saranga na kusababisha upigaji kura kutozingatia haki na taratibu.

Mwalimu amesema baadhi ya wananchi wameshindwa kupiga kura kutokana na majina yao kutoonekana vituoni wakati katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, walipiga kura katika vituo hivyo hivyo.

Mwenyekiti NEC atembelea vituo

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage ametembelea kituo cha kupigia kura  cha Leaders Club kuangalia upigaji kura unavyoendelea.

Amesema vituo vimefunguliwa kwa wakati na wapigakura wanaendelea kupiga kura katika kata nane na majimbo mawili yenye marudio ya uchaguzi.

Kuhusu malalamiko kwenye baadhi ya vituo vya kupiga kura amesema hadi sasa hajapokea malalamiko hayo na kwamba mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wanashirikiana vyema.

"Hadi sasa nimepokea malalamiko ya wakala mmoja kuwa na viapo viwili. Wakala anayemwakilisha mgombea mmoja hawezi kuwa na viapo viwili,” amesema Jaji Kaijage.

Alipoulizwa kuhusu viapo kucheleweshewa kwa mawakala wa vyama vya siasa amesema wakala anatakiwa kuwa na kiapo kabla ya muda wa uchaguzi kuanza ambapo wakala atatakiwa kuwa na barua ya utambulisho pamoja na kitambulisho.
Kifo cha Mwanafunzi aliyepigwa risasi chawagusa watu maarufu
 Taarifa za kifo cha mwanafunzi Aquillina Akwilini aliyepigwa risasi kifuani na Polisi na kupoteza maisha jana February 16, 2018 akiwa kwenye daladala zinaendelea kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Askari Polisi wakiwatawanya wafuasi wa upinzani waliokuwa wakifanya maandamano katika eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam.

Watu maarufu mbalimbali wameandika kwenye mitandao yao ya kijamii na kuonesha kuguswa na tukio hilo la kuuawa kwa Binti huyo, ikiwa ni pamoja na Mwanamuziki Shilole, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na Mwandishi wa Habari za Michezo Edo Kumwembe.

Saturday 3 February 2018

UN yaambiwa Korea Kaskazini inakiuka vikwazo
Ripoti ya waangalizi huru wa Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa Korea Kaskazini ilipata takriban dola milioni mia mbili mwaka uliopita kutokana na uuzaji wa bidhaa zilizopigwa marufuku katika mataifa ya nje huku ikikiuka vikwazo ilivyowekewa na jamii ya kimataifa.
Ripoti hiyo iliyovuja kutoka kwa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema kuwa nchi kadhaa zikiwemo, China, Urusi na Malaysia zilishindwa kuzuia uuzaji huo.
Inasemekana Korea Kaskazini ilituma shehena ya silaha hadi nchini Syria na Myanmar huku ikikiuka vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa.

Waangalizi hao pia walichunguza shehena ya mkaa iliyosafirishwa na meli ishirini hadi nchi jirani.
Balozi wa Myanmar katika Umoja wa Mataifa amesema taifa lake halina mkataba wowote wa silaha na Korea Kaskazini.

 Rais Kim Jong un

Aidha ripoti hiyo imenadi kuwa kampuni kadhaa za kimataifa za mafuta zilihusika kuiuzia Korea Kaskazini bidhaa zao.
Vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa vilivyotangazwa mwezi Disemba vilikadiriwa kupunguza ununuzi wa mafuta katika taifa hilo kwa asilimia 90 .
Vilishirikisha marufuku za bidhaa inazouza nje kama vile mashine na viufaa vya kielektroniki.
Wakati huohuo raia wote wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni waliagizwa kurudi nyumbani katika kipindi cha miezi 24.
Wachunguzi wa UN walibaini kwamba Myanmar na Syria zimekuwa zikishirikiana na Korea Kaskazini katika ununuzi wa silaha, Komid licha ya silaha hiyo kuorodheshwa katika vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo imesema kuwa kuna ushahidi kwamba Korea Kaskazini ilikuwa ikisaidia Syria kutengeza silaha za kemikali mbali na kuiuzia Myanmar silaha za masafa marefu.
Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni vimekuwa vikilenga biashara ya mkaa na China, bidhaa za kuuza nje zilizopigwa marufuku, vikwazo vya kusafiri, mali za watu binafsi na kampuni zinazohusishwa na mpango wa kinyuklia.
Picha: Lowassa alivyofika nyumba kwa Kingunge Kuhani Msiba
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema,Mheshimiwa Edward Lowassa akitia sahihi kwenye Kitabu cha  maombolezo nyumbani kwa Mzee Kingunge alipowasili jana jioni

Mbali na Lowassa pia walikuwepo viongozi wastaafu wa serikali kama Mzee Pius Msekwa na mkewe Mama Anna Abdalah,Waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa Salimu Ahmed Salimu,na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova.

Kingunge  alifariki alfajiri ya jana Ijumaa februari 02, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na kujeruhiwa na mbwa nyumbani kwake jijini Dar 
Mzee Kingune anatarajiwa kuzikwa Jumatatu 05,2018,katika Makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.