Monday, 26 March 2018

Watu 37 wafariki katika mkasa wa moto jumba la Kemerovo, Urusi
Watu 37 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la kibiashara katika mji maarufu kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi.

Watu zaidi ya 64 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto 41.

Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka.

Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry.

Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema.

Video zilizopakiwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka nje kupitia madirisha kujaribu kujinusuru kutoka kwa moto huo uliozuka Jumapili.

Wazima moto zaidi ya 660 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji.

Chanzo cha moto huo hakijabainika lakini maafisa wameanzisha uchunguzi.

Kemerovo, ni eneo maarufu sana kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe.

Ni mji unaopatikana takriban kilomita 3,600 mashariki mwa mji mkuu Moscow.

Kansela wa Austria Sebastian Kurz ametuma salamu zake za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waathiriwa, sawa na Waziri wa mambo ya nje wa Latvia Edgars Rinkēvičs.
 

Sunday, 25 March 2018

Mamilioni waandamana kutaka udhibiti wa bunduki Marekani
Mamilioni ya watu waliandamana katika miji mbalimbali ulimwenguni kote siku ya Jumamosi kushinikiza mageuzi katika sheria zinzohusu umiliki wa bunduki.

Kilele cha maandamano hayo yaliyopewa jina la March for our lives, ulikuwa ni mkutano uliohudhuriwa na takriban watu nusu milioni katika mji mkuu wa Marekani, Washington DC.

Maandamano hayo yalipangwa na shule ya upili ya Marjorie Stoneman Douglas mjini Parkland, jimbo la Florida, ambako watu wapatao 17, wakiwemo wanafunzi 14 walipoteza maisha yao kufuatia shambulizi la bunduki kwenye shule hiyo mapema mwaka huu.

Zaidi ya maandamano 800 yalikuwa yamepangwa kufanyika katika miji kadhaa ya Marekani na sehemu nyingine duniani kote, sambamba na yale ya mjini Washington DC.

Mashambulizi ya kutumia bunduki zenye nguvu, hususan kwenye shule Marekani yamezua mjadala mkali, huku wanasiasa wakitofautiana kuhusu hatua za kudhibiti matukio hayo.

Wanaharakati na wasanii maarufu walihudhuria maandamano hayo, wakiwemo wanamuziki Jennifer Hudson, Ariana Grande, Demi Lovato na Miley Cyrus.

Mjukuu wa mtetezi maarufu wa haki za binadamu Martin Luther King Jr, alishangiliwa kwa shangwe na vigelegele aliposimama kuhutubia mkutano wa Washington. Yolanda Renee King III alisema kizazi cha sasa ndicho kitaleta mabadiliko yanayohitajika.

"Na itoshe! Na itoshe!" alisema msichana huyo.

Kundi kubwa la waandamanaji baadaye lilionekana nje ya ikulu likibeba mabango licha ya kuwa rais Donald Trump hakuwemo wakati huo. Baadaye waliyaweka mabango yao chini na kuyaacha nje ya uzio wa ikulu kama ishara kwamba walitaka rais Trump asome ujumbe wao.

Thursday, 22 March 2018

Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook:- Part Two Mwendelezo
Usibonyeze kitufe cha 'like' katika ukurasa wa bidhaa na iwapo unataka kucheza michezo ama mitahani usiingie kupitia facebook badala yake ingia moja kwa moja katika tovuti hiyo , amesema Paul Bernal muhadhiri wa habari na teknolojia katika chuo cha kusomea sheria cha East Anglia School.

''Ni rahisi kupitia akaunti yako ya facebook , lakini kufanya hivyo kunampatia uwezo mwenye programu hiyo kuona habari nyingi katika ratiba yako ya data'' , aliongezea.
Ni njia ipi nyengine inayoweza kulinda data yako katika facebook?

Kuna njia moja pekee inayoweza kukuhakikisha kuwa data yako haionekani na mtu mwengine kulingana na Bernal. 'Ondoka Facebook'.

''Facebook itaweza kuwalinda zaidi wateja wake iwapo wataanza kuondoka katika mtandao huo. Kwa sasa kuna uwezekano mchache kufanya mabadiliko hayo'', aliambia BBC.

Inaonekana hayupo pekee katika wito huo wa kutoka Facebook.Ujumbe wenye alama ya reli #DeleteFacebook umesambazwa sana katika mtandao wa Twitter kufuatia kashfa hiyo ya Cambridge Analytica .

Lakini Bernal anajua kwamba ni watu wachache watakaotoka katika mtandao huo hususan wale wanaoona facebook kuwa muundo msingi wa maisha yao.

Je unaweza kubaini ni habari gani zinazokuhusu zimehifadhiwa?

FAHAMU Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook

Madai kwamba kampuni ya utafiti ya Cambridge Analytica ilitumia vibaya data ya watu milioni 50 wanaotumia Facebook yamefungua mjadala kuhusu ni vipi habari zilizopo katika mtandao huo wa kijamii husambazwa na kwa nani.
Data ni kama mafuta katika mtandao wa facebook, ndio kivutio kikuu cha matangazo ya biashara kwa mtandao huo ambao hujipatia faida kubwa.

Hakuna shaka kwamba facebook ina uwezo wa kujenga habari kuhusu wateja wake kwa mfano wanachopenda, wasichopenda maisha yao na mirengo yao ya kisiasa.
Swali kuu ni nini wanachosambaza kwa watu wengine na ni nini ambacho watumiaji wanaweza kufanya ili kudhibiti habari zao?.
Tumeona mitihani inayotaka kupima fikra, kufichua wewe ni nani ama hata kuonyesha ni nini ungependa iwapo wewe ni muigizaji anayependeza.
Ulikuwa ujumbe kutoka kwa mtihani mmoja wa facebook - Huu ndio ujumbe wa kidijitali uliodaiwa kutumiwa kuvuna habari za mamilioni ya watu. Mitihani kama hiyo hufanyika kwa hakikisho kuwa data yako iko salama.

Michezo hii na mitihani inalenga kuwavutia wateja wa facebook na inakubalika na masharti ya mtandao huo.

facebook imebadilisha masharti yake kupunguza habari ambazo kampuni nyengine inaweza kuchukua hususan kuwazuia kuchukua habari kuhusu marafiki wa wateja wake.

Bado haijajulikani ni habari gani zilizochukuliwa -hilo ni swala linalochunguzwa na mamlaka ya ulinzi wa data nchini Uingreza ICO.

Nini ambacho wateja wa facebook wanaweza kufanya ili kulinda data yao?

    Ingia katika facebook na kutembelea Programu iliopo katika ukurasa wa setting

    Bonyeza kitufe cha edit chini ya programu, tovuti na Plugins

    Haribu programu iliopo

Hii inamaanisha kwamba hautaweza kutumia watumiaji wa facebook ambao sio marafiki zako na iwapo hiyo ni hatua kubwa kuna njia ya kuzuia kiwango cha habari zitakazotumiwa na programu wakati unapozitumia.

    Ingia katika ukurasa wa programu ya setting
    Bonyeza kila orodha ambayo huitaki programu yako kuona ikiwemo bio, siku ya kuzaliwa, familia, dini, iwapo uko katika mtandao , machapisho katika ratiba yako ya data, vitendo na maslahi yako.
Mmiliki wa facebook aomba radhi kwa kashfa ya Analytica
Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica,ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa. Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

AmesemaThe CEO said: "Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu,na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia,mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook,mwisho wa siku nina wajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu."Amesema Zuckerberg.

Nini ambazo Zuckerberg ameahidi kukifanya?

Katika kufuatilia matatizo ya sasa nay a zamani amesema atafanya mambo yafuatayo

Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko yam waka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.

Kufanyia uchunguzi kazi za program za kimitandao zinazotiliwa shaka

Kupiga marufuku mwanzilishi wa program yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zita pafanya Facebook kuwa mahala salama.

Tuesday, 20 March 2018

Mkurugenzi wa FBI aliyefutwa kazi 'amwaga mtama' kuhusu mazungumzo na Trump
   

Naibu mkurugenzi wa zamani katika shirika la ujasusi nchini Marekani FBI Andrew McCabe ametoa barua kuhusu mazungumzo aliyokuwa nayo na rais wa Marekani Donald Trump kwa kamati inayochunguza 'mkono' wa Urusi katika uchaguzi wa urais wa 2016 , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Barua hizo huenda zikasaidia madai kwamba rais Trump alitaka kuzuia haki kufanyika. Bwana McCabe alifutwa kazi katika shirika la FBI siku ya Ijumaa .

Bwana Trump alimtuhumu kwa kufanya upendeleo na kusema siku ya Jumapili kwamba Bwana McCabe hakuandika walichokuwa wakizungumzia.
Rais huyo pia alipuuzilia mbali uchunguzi huo wa Urusi akisema kuwa 'anaandmwa kisiasa'. Uchunguzi huo unaongozwa na wakili maalum Robert Mueller ,ambaye ni mkurugenzi wa zamani wa FBI .

Kufikia sasa amewashtaki watu 19. Wakili wa rais John Dowd alitoa taarifa siku ya Jumamosi akisema kuwa ni wakati uchunguzi huo wa wakili maalum unafaa kutamatishwa.

Bwana Trump amelalamika kwamba kundi hilo la Mueller linashirikisha wanachama 13 wa chama cha Democrats , wafuasi wa Hillary Clinton na hakuna wananchama wa Republicans.
 
https://twitter.com/realDonaldTrump
 
  Kwa nini McCabe alifutwa kazi na Trump?

Bwana McCabe alikuwa akichunguzwa na FBI na alikuwa tayari amejiondoa kwa muda katika wadhfa wake mnamo mwezi Januari akisubiri matokeo ya uchunguzi huo.

Alipigwa kalamu siku mbili kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya 50 siku ya Jumapili alipotarajiwa kustaafu kupitia pensheni ya kijimbo.

Mwanasheria mkuu Jeff Session alisema kuwa uchunguzi ulisema kuwa bwana McCabe alitoa matamshi yasiofaa chini ya kiapo mara kadhaa.