Thursday 22 March 2018

Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook:- Part Two Mwendelezo

Usibonyeze kitufe cha 'like' katika ukurasa wa bidhaa na iwapo unataka kucheza michezo ama mitahani usiingie kupitia facebook badala yake ingia moja kwa moja katika tovuti hiyo , amesema Paul Bernal muhadhiri wa habari na teknolojia katika chuo cha kusomea sheria cha East Anglia School.

''Ni rahisi kupitia akaunti yako ya facebook , lakini kufanya hivyo kunampatia uwezo mwenye programu hiyo kuona habari nyingi katika ratiba yako ya data'' , aliongezea.
Ni njia ipi nyengine inayoweza kulinda data yako katika facebook?

Kuna njia moja pekee inayoweza kukuhakikisha kuwa data yako haionekani na mtu mwengine kulingana na Bernal. 'Ondoka Facebook'.

''Facebook itaweza kuwalinda zaidi wateja wake iwapo wataanza kuondoka katika mtandao huo. Kwa sasa kuna uwezekano mchache kufanya mabadiliko hayo'', aliambia BBC.

Inaonekana hayupo pekee katika wito huo wa kutoka Facebook.Ujumbe wenye alama ya reli #DeleteFacebook umesambazwa sana katika mtandao wa Twitter kufuatia kashfa hiyo ya Cambridge Analytica .

Lakini Bernal anajua kwamba ni watu wachache watakaotoka katika mtandao huo hususan wale wanaoona facebook kuwa muundo msingi wa maisha yao.

Je unaweza kubaini ni habari gani zinazokuhusu zimehifadhiwa?

0 comments: