Tuesday 20 March 2018

Mkurugenzi wa FBI aliyefutwa kazi 'amwaga mtama' kuhusu mazungumzo na Trump

   

Naibu mkurugenzi wa zamani katika shirika la ujasusi nchini Marekani FBI Andrew McCabe ametoa barua kuhusu mazungumzo aliyokuwa nayo na rais wa Marekani Donald Trump kwa kamati inayochunguza 'mkono' wa Urusi katika uchaguzi wa urais wa 2016 , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Barua hizo huenda zikasaidia madai kwamba rais Trump alitaka kuzuia haki kufanyika. Bwana McCabe alifutwa kazi katika shirika la FBI siku ya Ijumaa .

Bwana Trump alimtuhumu kwa kufanya upendeleo na kusema siku ya Jumapili kwamba Bwana McCabe hakuandika walichokuwa wakizungumzia.
Rais huyo pia alipuuzilia mbali uchunguzi huo wa Urusi akisema kuwa 'anaandmwa kisiasa'. Uchunguzi huo unaongozwa na wakili maalum Robert Mueller ,ambaye ni mkurugenzi wa zamani wa FBI .

Kufikia sasa amewashtaki watu 19. Wakili wa rais John Dowd alitoa taarifa siku ya Jumamosi akisema kuwa ni wakati uchunguzi huo wa wakili maalum unafaa kutamatishwa.

Bwana Trump amelalamika kwamba kundi hilo la Mueller linashirikisha wanachama 13 wa chama cha Democrats , wafuasi wa Hillary Clinton na hakuna wananchama wa Republicans.
 
https://twitter.com/realDonaldTrump
 
  Kwa nini McCabe alifutwa kazi na Trump?

Bwana McCabe alikuwa akichunguzwa na FBI na alikuwa tayari amejiondoa kwa muda katika wadhfa wake mnamo mwezi Januari akisubiri matokeo ya uchunguzi huo.

Alipigwa kalamu siku mbili kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya 50 siku ya Jumapili alipotarajiwa kustaafu kupitia pensheni ya kijimbo.

Mwanasheria mkuu Jeff Session alisema kuwa uchunguzi ulisema kuwa bwana McCabe alitoa matamshi yasiofaa chini ya kiapo mara kadhaa.


0 comments: