Sunday, 25 March 2018

Mamilioni waandamana kutaka udhibiti wa bunduki Marekani
Mamilioni ya watu waliandamana katika miji mbalimbali ulimwenguni kote siku ya Jumamosi kushinikiza mageuzi katika sheria zinzohusu umiliki wa bunduki.

Kilele cha maandamano hayo yaliyopewa jina la March for our lives, ulikuwa ni mkutano uliohudhuriwa na takriban watu nusu milioni katika mji mkuu wa Marekani, Washington DC.

Maandamano hayo yalipangwa na shule ya upili ya Marjorie Stoneman Douglas mjini Parkland, jimbo la Florida, ambako watu wapatao 17, wakiwemo wanafunzi 14 walipoteza maisha yao kufuatia shambulizi la bunduki kwenye shule hiyo mapema mwaka huu.

Zaidi ya maandamano 800 yalikuwa yamepangwa kufanyika katika miji kadhaa ya Marekani na sehemu nyingine duniani kote, sambamba na yale ya mjini Washington DC.

Mashambulizi ya kutumia bunduki zenye nguvu, hususan kwenye shule Marekani yamezua mjadala mkali, huku wanasiasa wakitofautiana kuhusu hatua za kudhibiti matukio hayo.

Wanaharakati na wasanii maarufu walihudhuria maandamano hayo, wakiwemo wanamuziki Jennifer Hudson, Ariana Grande, Demi Lovato na Miley Cyrus.

Mjukuu wa mtetezi maarufu wa haki za binadamu Martin Luther King Jr, alishangiliwa kwa shangwe na vigelegele aliposimama kuhutubia mkutano wa Washington. Yolanda Renee King III alisema kizazi cha sasa ndicho kitaleta mabadiliko yanayohitajika.

"Na itoshe! Na itoshe!" alisema msichana huyo.

Kundi kubwa la waandamanaji baadaye lilionekana nje ya ikulu likibeba mabango licha ya kuwa rais Donald Trump hakuwemo wakati huo. Baadaye waliyaweka mabango yao chini na kuyaacha nje ya uzio wa ikulu kama ishara kwamba walitaka rais Trump asome ujumbe wao.

Friday, 23 March 2018

Ifahamu Afya yako kupitia Rangi ya Mkojo wako
Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu  afya yako? Kama jibu ni hapana basi makala haya yanakusu wewe, kwani rangi ya mkoja kwa mujibu wa watalamu wa afya unauwezo mkubwa wa kukuoa ukweli juu ya afya yako.

1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):
Unakunywa maji mengi.

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo. Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.

3. Manjano iliyo pauka.Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha

4. Njano iliyo kolea. Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali. Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.

6. Rangi ya Kahawia. Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kamali hii ikiendelea.

7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu. Kama hujala matunda yoyote yenye asili ya uwekundu, basi huwenda una famu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.


Thursday, 22 March 2018

Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook:- Part Two Mwendelezo
Usibonyeze kitufe cha 'like' katika ukurasa wa bidhaa na iwapo unataka kucheza michezo ama mitahani usiingie kupitia facebook badala yake ingia moja kwa moja katika tovuti hiyo , amesema Paul Bernal muhadhiri wa habari na teknolojia katika chuo cha kusomea sheria cha East Anglia School.

''Ni rahisi kupitia akaunti yako ya facebook , lakini kufanya hivyo kunampatia uwezo mwenye programu hiyo kuona habari nyingi katika ratiba yako ya data'' , aliongezea.
Ni njia ipi nyengine inayoweza kulinda data yako katika facebook?

Kuna njia moja pekee inayoweza kukuhakikisha kuwa data yako haionekani na mtu mwengine kulingana na Bernal. 'Ondoka Facebook'.

''Facebook itaweza kuwalinda zaidi wateja wake iwapo wataanza kuondoka katika mtandao huo. Kwa sasa kuna uwezekano mchache kufanya mabadiliko hayo'', aliambia BBC.

Inaonekana hayupo pekee katika wito huo wa kutoka Facebook.Ujumbe wenye alama ya reli #DeleteFacebook umesambazwa sana katika mtandao wa Twitter kufuatia kashfa hiyo ya Cambridge Analytica .

Lakini Bernal anajua kwamba ni watu wachache watakaotoka katika mtandao huo hususan wale wanaoona facebook kuwa muundo msingi wa maisha yao.

Je unaweza kubaini ni habari gani zinazokuhusu zimehifadhiwa?

FAHAMU Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook

Madai kwamba kampuni ya utafiti ya Cambridge Analytica ilitumia vibaya data ya watu milioni 50 wanaotumia Facebook yamefungua mjadala kuhusu ni vipi habari zilizopo katika mtandao huo wa kijamii husambazwa na kwa nani.
Data ni kama mafuta katika mtandao wa facebook, ndio kivutio kikuu cha matangazo ya biashara kwa mtandao huo ambao hujipatia faida kubwa.

Hakuna shaka kwamba facebook ina uwezo wa kujenga habari kuhusu wateja wake kwa mfano wanachopenda, wasichopenda maisha yao na mirengo yao ya kisiasa.
Swali kuu ni nini wanachosambaza kwa watu wengine na ni nini ambacho watumiaji wanaweza kufanya ili kudhibiti habari zao?.
Tumeona mitihani inayotaka kupima fikra, kufichua wewe ni nani ama hata kuonyesha ni nini ungependa iwapo wewe ni muigizaji anayependeza.
Ulikuwa ujumbe kutoka kwa mtihani mmoja wa facebook - Huu ndio ujumbe wa kidijitali uliodaiwa kutumiwa kuvuna habari za mamilioni ya watu. Mitihani kama hiyo hufanyika kwa hakikisho kuwa data yako iko salama.

Michezo hii na mitihani inalenga kuwavutia wateja wa facebook na inakubalika na masharti ya mtandao huo.

facebook imebadilisha masharti yake kupunguza habari ambazo kampuni nyengine inaweza kuchukua hususan kuwazuia kuchukua habari kuhusu marafiki wa wateja wake.

Bado haijajulikani ni habari gani zilizochukuliwa -hilo ni swala linalochunguzwa na mamlaka ya ulinzi wa data nchini Uingreza ICO.

Nini ambacho wateja wa facebook wanaweza kufanya ili kulinda data yao?

    Ingia katika facebook na kutembelea Programu iliopo katika ukurasa wa setting

    Bonyeza kitufe cha edit chini ya programu, tovuti na Plugins

    Haribu programu iliopo

Hii inamaanisha kwamba hautaweza kutumia watumiaji wa facebook ambao sio marafiki zako na iwapo hiyo ni hatua kubwa kuna njia ya kuzuia kiwango cha habari zitakazotumiwa na programu wakati unapozitumia.

    Ingia katika ukurasa wa programu ya setting
    Bonyeza kila orodha ambayo huitaki programu yako kuona ikiwemo bio, siku ya kuzaliwa, familia, dini, iwapo uko katika mtandao , machapisho katika ratiba yako ya data, vitendo na maslahi yako.
TCRA, Mwakyembe Wamkabili Diamond




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam.

 Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.

Katika mahojiano hayo, Diamond alimjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutokana na Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Kisaka amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.

Amesema suala hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na kamati ya maudhui na kuahidi kulitolea ufafanuzi siku za hivi karibuni akiwataka wananchi kuwa na subira.

Wakati TCRA ikisema hivyo, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema amesikitishwa na matamshi ya Diamond kuhusu kufungiwa kwa nyimbo hizo aliyoyatoa katika kipindi hicho.

“Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo za wasanii wawili kwa kukiuka maadili yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Shonza ambaye analaumiwa na Diamond,” amesema.

“Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake na maamuzi ya naibu waziri ni ya wizara. Kama vikao na wasanii tumefanya vingi sana, lakini Diamond hakuwahi kuhudhuria vikao hivyo, si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao cha peke yake.”

Amesisitiza, “Sheria ni ya watu wote bila kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii, hivyo msanii Diamond anapaswa kutii sheria na mamlaka zilizowekwa.”

Dk Mwakyembe ameeleza kuwa sio busara kwa Diamond  kushindana na Serikali na endapo ana ushauri wowote ni vyema akawasilisha kwa njia sahihi, lakini si kumshambulia naibu waziri kwa dharau na kejeli kama alivyofanya.

“Diamond kwa mafanikio aliyoyapata katika muziki, anatarajiwa kuwa mfano bora kwa wanamuziki wenzake. Napenda kuwakumbusha wasanii wote kwamba sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine,” amesema.

“Pamoja na kuwa na kipaji hicho, wasanii wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia tasnia ya sanaa kama ilivyo kwa tasnia nyingine.”